Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele aitanguliza Yanga kwa Mkapa

Mayele  Makambo Mayele aitanguliza Yanga kwa Mkapa

Sat, 25 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

DAKIKA 45 zimemalizika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa huku Yanga wakienda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Simba.

Yanga ilipata bao dakika 13 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake Fiston Mayele kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Simba Aishi Manula.

Yanga ilianza mchezo kwa umakini mkubwa kwa kulishambulia lango la Simba dakika 10, za mwanzo kabla ya Simba kujibu mapigo ya kulishambulia lango la Yanga bila ya kupata mafanikio yeyote.

Katika mchezo wa leo eneo kubwa ambalo limeonekana kuwa na ushindani ni eneo la katikati ya Uwanja kati ya waganda wawili Khalid Aucho ambaye ndiye mchezo wake wa kwanza wa dabi dhidi ya Taddeo Lwanga.

Licha ya umahiri wa kupandisha mashambulizi kwa mabeki Shomari Kapombe kwa upande wa Simba na Shaban Djuma wa Yanga, ila bado timu zote zinaonekana kutumia mipira zaidi kwenye eneo la kiungo.

Kocha wa Simba Didier Gomes ilimlazimu kufanya mabadiliko yasiyokuwa ya kiufundi kwa kumuingiza beki Kenneth Juma akichukua nafasi ya Mkenya Joash Onyango dakika ya 31.

Onyango alipata majeraha ya kichwa  baada ya kugongana na mchezaji mwenzake Chris Mugalu wakati wa harakati za kuwania mpira.

Licha ya ubabe mwingi uliotawala katika mchezo wa leo ila mwamuzi Ramadhan Kayoko ameonekana kulimudu pambano kwa kwa kiasi kikubwa katika dakika hizi 45 za kipindi cha kwanza.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz