Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele aitaka Rekodi ya Gwiji huyu Yanga

Fiston Kalala Mayele 15 Goals Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ameweka wazi kutamani rekodi iliyowekwa na nyota wa zamani wa kikosi hicho, Mohamed Hussein 'Mmachinga' ya kufikisha mabao 26 ndani ya msimu mmoja.

Nyota huyo ambaye ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa amefunga 15 katika michezo 23 aliyocheza hadi sasa amezungumza hayo wakati mabingwa hao watetezi wakijiandaa na mchezo dhidi ya Geita Gold utakaopigwa kesho Uwanja wa Azam Complex.

"Mshambuliaji lazima uwe na malengo binafsi, natamani Kufikia rekodi ya Mmachinga na mechi saba zilizobaki siwezi kusema nitafunga mabao 15 nifikishe 30 ingawa nitaendelea kupambana na mwenyezi Mungu akipenda nitachukua kiatu," amesema na kuongeza;

"Kwanza binafsi muhimu sana ni malengo ya timu kwa sababu tunataka kuchukua ubingwa tena kwa msimu huu mwingine," amesema.

Aidha Mayele ameelezea furaha yake ya kuchaguliwa Kwenye timu ya taifa ya Congo licha ya kuwa na mastaa wengi wanaocheza ulaya.

"Nimeitwa timu ya taifa ya Congo kwa mara ya kwanza hivyo natoa shukrani kwa timu ya Yanga na benchi la ufundi kwa kunipa nafasi ya kuonekana."

Msimu uliopita nyota huyo alimaliza na mabao 16 nyuma ya aliyekuwa mshambuliaji wa Geita Gold, George Mpole aliyemaliza kinara na mabao 17.

Chanzo: Mwanaspoti