Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele aisaidia Pyramids kupata alama tatu

Mayele M5238 Mayele aisaidia Pyramids kupata alama tatu

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fiston Mayele hapo jana aliingia Dimbani dakika ya 59 kuchukua nafasi ya Fargie Lakay wakati huo Pyramids Football Club walikuwa Bado hawajapata bao dhidi ya Al Ittihad katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri.

Baada ya Mayele kuingia Pyramids walichangamka zaidi na kupata bao dakika ya 75 Ahmed Sammy dakika ya 75 na kusepa na alama tatu muhimu (1-0).

Kazi nzuri ya Fiston Mayele, Mohamed Chibi na Ahmed Sammy inawapa alama tatu vijana wa Pyramids ambao wanachupa Hadi nafasi ya tatu kunako msimamo wa EPL.

Msimamo wa EPL:

1. ENPPI - 23 pts

2. ZED - 21 pts

3. Pyramids FC - 21 pts

4. Al Ittihad - 19 pts

Al Ahly Sporting Club wamecheza michezo 6 wakati Zamalek Sporting Club wakishuka Dimbani mara 8, kinara wa Ligi ENPPI wameshuka Dimbani mara 13 hivyo Pyramids, Zamalek na Al Ahly wakishinda michezo yao watarudi juu tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live