Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele aibukia KenGold

Mayele Kassim Mayele aibukia KenGold

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya KenGold imekamilisha usajili wa aliyekuwa mshambuliaji wa Green Warriors, Kassim Shaibu ‘Mayele’ kwa mkataba wa miezi sita huku nyota huyo akikiri licha ya kubadilisha mazingira ila shauku yake kubwa ni kuendelea kufanya vizuri.

Nyota huyo mwenye mabao manane katika Ligi ya Championship alisema ni furaha kubwa kwake kujiunga na timu hiyo ya jijini Mbeya huku akiomba ushirikiano kuanzia kwa wachezaji wenzake na viongozi ili kufikia malengo ya kupanda Ligi Kuu Bara.

“Nawashukuru sana viongozi wa KenGold kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuichezea timu hii, kwangu ni deni kubwa ambalo naamini napaswa kulilipa uwanjani kwa kuendelea kuonyesha kiwango kizuri kama nilivyokuwa nafanya nilikotoka,” alisema.

Kwa upande wa kocha mkuu wa timu hiyo, Jumanne Challe alisema ongezeko la nyota huyo litaleta tija ndani ya kikosi hicho kutokana na ubora alionao huku akiweka wazi eneo la ushambuliaji limeimarika zaidi kutokana na washambuliaji waliopo.

Mayele anaungana kwenye timu hiyo na mfungaji kinara hadi sasa katika Ligi ya Championship, Edgar William mwenye mabao 13.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live