Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele afichua alivyomzuia Feisal asiondoke Yanga

Feisal Na Mayele Mayele afichua alivyomzuia Feisal asiondoke Yanga

Tue, 8 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Fiston Mayele, amefunguka kuwa, wakati Feisa Salum alipotaka kuondoka Yanga, alimshauri asiondoke.

Hilo limejidhirisha kupitia documentary ya Yanga waliyoizindua hapoa jana Agosti 7, 2023.

“Mimi Feisal ni rafiki yangu, najua mambo yake anajua mambo yangu, nakumbuka maneno ya yeye kuondoka Yanga alianza kuniambia wakati tunaenda kucheza mechi ya marudiano na Club Africain.

“Lakini mimi nilimwambia usiondoke wakati huu (ule), subiri msimu uishe ndio uondoke, nilimwambia wewe umecheza hii Timu kwa muda mrefu subiri huu msimu uishe ndio uondoke,” Fiston Mayele akizungumza kwenye Documentary ya Yanga Sc.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live