Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele: Tumesikia kilio cha Wananchi, tumeshapata dawa ya Ibenge

Mayele Feisal Ethiopia Mayele: Tumesikia kilio cha mashabiki, tumeshapata dawa ya Ibenge

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika kiongozi wa Yanga SC, Fiston Mayele amesema wachezaji na bechi la ufundi la timu hiyo wameyasikia maneno kutoka kwa mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuelekea mechi yao ya mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Hilal ya Sudan.

Mayele amesema hayo akiwa Addis Ababa nchini Ethiopia pamoja na kikosi cha wachezaji wenzake 24 wakielekea Khartoum-Sudan kwa ajili mchezo huo kama wachezaji hawana jingine zaidi ya kupata ushindi katika mechi hiyo.

"Tumepata habari zote kutoka kwa mashabiki na Wanachama wa Yanga wanataka timu yao iingie makundi, na sisi kama wachezaji tutahakikisha tunapambana kutimiza hilo na kuwapa furaha mashabiki zetu.

"Tuna fahamu hauta mchezo rahisi, lakini tutahakikisha tunapata matokeo kwa sababu hakuna kingine zaidi ya kupata matokeo. Lazima tufunge ili tuwe na uhakika wa kusonga mbele, tusipofunga maana yake tunatolewa.

"Mechi ya kwanza hapa nyumbani ilikuwa ngumu kwa sababu tunamjua Ibenge ni mtu wa ku-block, ndio maana nilipokuwa nikishuka kuchukua mipira nyuma yangu kuna watu wawili. Kwa hiyo anapenda sana ku-block na kuzuia, hata goli nililofunga ni la mbali.

"Mechi ya hapa kwetu tulipata nafasi nyingi sana lakini tulishindwa kuzitumia ipasavyo, walimu wameshalifanyia kazi hilo na tumerekebisha makosa hayo, kwa hiyo tutahakikisha nafasi tunazopata tunazitumua vizuri kupata matokeo.

"Lakini mechi ya nyumbani na yeye atataka kucheza na si kupaki basi, kwa hiyo na sisi tutatumia mafasi hiyo kucheza na kupata matokeo chanya," amesema Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live