Aliyekuwa mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa aligoma kucheza mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (wakati huo) msimu uliopita ili akacheze kwenye timu yake ya Taifa ya Congo.
Hayo ameyasema Fiston Mayele ambaye kwa sasa yupo Pyramids FC ya Misri, katika mahojiano na Azam TV akielezea alivyofurahia kuitwa timu ya Taifa ya nchi yake, jambo ambalo lilikuwa ndoto yake ya muda mrefu.
"Mwaka jana nilikataa kwenda kucheza mechi ya fainali (ya Kombe la Shirikisho la TFF) ya Yanga na Azam kwa sababu ile mechi ningeicheza, mechi ya Gabon (dhidi ya DR Congo) nisingetakiwa kuicheza."
Hata hivyo, amesema kushindwa kupata muda wa kutosha kucheza kwenye AFCON kumetokana na nchi yake kuwa na wachezaji wengi wazuri, hasa washambuliaji ambao wanacheza Ulaya.