Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele: Nikirudi Yanga mashabiki watanipokea tu

Mayele Hersi A0002 Fiston Mayele

Sun, 26 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msikie mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele raia wa Congo DR ambaye kwa sasa anasakata kabumbu la kulipwa Pyramids FC ya Misri.

"Pamoja na kwamba kumekuwa na vita kubwa juu yangu kwenye mitandao ya kijamii, bado naamini kwa asilimia 100% kwamba nikirudi Yanga mashabiki watanipokea.

"Kitu ambacho nimejifunza Tanzania ni kwamba mashabiki wengi huwa wanajali maslahi yao na sio ya wachezaji.

"Kucheza misimu miwili ndani ya yanga ilikuwa ni furaha sana kwao, ila ilipofika hatua ya mimi kuondoka, watu walianza kunichukia bila sababu yoyote.

"Mbona wachezaji wengi tuu wanaenda pale na kuondoka ila mimi tuu ndo wawe na chuki kubwa na mimi!!?, kosa langu kubwa liko wapi?

"Japo kuwa naamini kabisa nikirudi napokelewa kwa sababu narudisha maslahi kwenye upande wa timu na mashabiki, ila sidhani kama wanachokifanya ni sahihi," amesema Mshambuliaji wa zamani wa @yangasc Fiston Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live