Mshambuliaji kinara wa Yanga, Fiston Kalala Mayele amesema wamejiandaa kwenda kupambana ili kupata matokeo dhidi ya klabu ya Real Bamako nchini Mali.
Mayele amesema hayo alfajiri ya leo Alhamisi, Februari 23, 2023 wakati akiondoka na kikosi chake kuelekea Mali kwa ajili ya mchezo wa kundi D wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
“Tunaenda leo lakini mechi itakuwa Jumapili. Baada ya kupoteza ule mchezo wa Tunisia tulijipanga vizuri kupata alama tatu nyumbani, tunamshukuru Mungu tulipata poini tatu. Hapa tunakwenda ugenini kupambani timu yetu, alama tatu tulizopata Jumapili zitatusaidia.
“Mechi ya kwanza ya Tunisia tulifanya makossa tukafungwa mabao mawili ya mipira iliyokufa, tuliporudi nyumbani tulitumia makossa yetu kujifunza na kuboresha, hata sisi washambuliaji nadhani mliona mechi ya mazembe tuliboresha tukapata ushindi.
“Malengo ya timu ni kwenda mbali kimataifa, na sisi pia wachezaji tunatamni kufanya vizuri kimataifa. Mungu akijalia tutabeba ubingwa," amesema Mayele.
Katika Kundi D la Kombe la Shirikisho, US Monastir ya Tunisia wanaongoza wakiwa na alama 4, wakifuatiwa na Yanga wenye alama 3, TP Mazembe alama 3 na Real Bamako akivuta mkia na alama 1.