Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Fiston Mayele ameelezwa kushangazwa na watu wanataka aondoke Yanga na kwenda timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba na klabu hiyo.
Mayele ameeleza hayo wakati akihojiwa na Manara TV mara baada ya mchezo wa hisani kati ya Timu Job na Timu Kibwana kumalizika mjini Morogoro jana, Iju.aa.
"Wakati nakuja hapa Tanzania hakuna mtu aliyenijua, nilichokifanya ni kujituma na nidhamu. Ninaipenda kazi yangu ndio maana leo kila mtu anamuimba Mayele.
"Nilisema tangu nikiwa mdogo malengo yangu ni kucheza mpira na nitafanikiwa kupitia soka, kwa sasa naona nimeanza kutimiza malengo yangu na kupata japo mafanikio lakini sijafikia hata nusu ya malengo yangu, nitaendelea kuoambana zaidi.
"Ninawashangaa wanaotaka niondoke Yanga, watu wanasubiri kwa hamu 'Thank You' ya Mayele, mimi bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Yanga na ninaheshimu mkataba wangu, ikija ofa tutakaa mezani tutazungumza," amesema Mayele.
Raisi wa Yanga Injinia Hersi Said amesema jukumu la uongozi wake ni kuhakikisha wanawabakisha wachezaji wote muhimu kikosini
Tayari Yanga wamempa Mayele ofa ya mkataba mpya kukiwa na maboresho ya mshahara wake hata hivyo Yanga imeweka wazi msimamo wake kuwa iko tayari kuzingatia maamuzi yenye maslahi kwa pande zote mbili ikitokea timu imewasilisha ofa nono zaidi.