Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele: Morocco wepesi, Tanzania hatukuwapania

Mayele Vs Morocco Mayele: Morocco wepesi, Tanzania hatukuwapania

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Congo DR Fiston Mayele amesema kwao Morocco ni Timu nyepesi tofauti na Egypt ambayo iliwapa wakati mgumu hadi kufanikiwa kuitoa kwenye mashindano ya AFCON usiku wa kuamkia leo.

Akiongea kwa furaha baada ya kuitoa Egypt kwa penati, Mayele amenukuliwa akisema

"Jamani siwezi kujisahau hii ndio Congo, hakuna Mtu ambaye alikua anategemea kama sisi tungemtoa Misri na tumemtoa leo kesho anarudi nyumbani, so kusema sisi tulipania mechi ya Tanzania tunapania vipi bwana ? Mbona Morocco wepesi, Misri wana Timu kubwa wana Timu nzuri sana wametuhangaisha"

"Ndugu zangu Watanzania mimi nawapenda sana, ndio Nchi yangu ya pili... nadhani nusu ya Watanzania walikua nyuma yetu, leo ni siku kubwa kwetu siku ya furaha, sina maneno wallah, wallah sina maneno"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live