Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele, Fei Toto wamtesa kocha Zalan

MAYELE Na FEI TOTO (1) Mayele, Fei Toto wamtesa kocha Zalan

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Zalan, Mawein Deng amewataja Fiston Mayele na Feisal Salam ‘Feitoto’ kuwa ndio wachezaji anaowahofia zaidi hapo kesho.

Wawili hao ndio walio wafunga kwenye ushindi wa mabao 4-0 huku Mayele akiingia kambani mara 3 na Fei Toto akifunga bao moja.

Akizungumzia mchezo kwa ujumla alisema timu yake imefanyia kazi makosa waliyoyafanya kwenye mchezo uliopita wamejiandaa vizuri kwa mchezo wa kesho.

“Tunatarajia mchezo mzuri na wa ushindani tumejiandaa kushindana lolote linaweza kutokea Yanga ni timu kubwa inawachezaji wengi wazuri lakini tunahofia zaidi mchezaji aliyevaa jezi namba 9 (Mayele) na namba 6 (Fei Toto),” alisema na kuongeza.

“Tumekuja kupambana tutapambana hadi dakika ya mwisho bado tuna nafasi ya kufanya kitu  dakika 90 ndio zitaamua nani anatakiwa kuendelea hatua inayofuata,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live