Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele, Baraza wang'ara tuzo za Mwezi

FK N MxWUAE7Wd Fiston Mayele, Mchezaji Bora wa Mwezi Januari

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji Mkongo wa Yanga SC, Fiston Kalala Mayele ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mwezi Januari, huku Francis Baraza wa Kagera Sugar akiwa Kocha Bora.

Kwa mwezi Januari, Mayele amecheza michezo miwili akiwa na Yanga na yote waliibuka na ushindi huku akipachika goli moja na kutoa pasi moja ya Bao.

Mayele amewashinda Reliant Lusajo wa Namungo na Tepsi Evans wa Azam FC.

Kwa Upande wa Kocha bora wa Mwezi Januari, Kocha wa Kagera Sugar Francis Baraza aliwashinda Nasreddine Nabi na Mathias Lule wa Mbeya City. Kagera Sugar imecheza michezo mitatu ikishinda dhidi ya Simba na Dodoma Jiji, Kisha ikatoa sare na Biashara United.



Katika hatua nyingine Kamati ya Tuzo imemteua Meneja wa Uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa John Nzwalla kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Januari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live