Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele, Aziz KI wapewa ujanja

Yanga Mayeleeeh Mayele, Aziz KI wapewa ujanja

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Winga wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Ulimboka Mwakingwe ‘Uli’ amesema Yanga ina nafasi ya kufanya vizuri kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini tu ikijua kutofautisha ligi na michuano ya kimataifa na kuwapa ujanja mastaa wa timu hiyo.

Yanga itashuka uwanja Jumapili kuvaana na TP Mazembe ya DR Congo katika mechi ya pili ya Kundi D ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya awali kupoteza 2-0 ugenini kwa US Monastir ya Tunisia.

Ulimboka aliyeitazama mechi ya kwanza ya jijini Tunis, alisema mastaa wa Yanga wakiongozwa na Stephane Aziz KI, Fiston Mayele na Khalid Aucho walishindwa kucheza kwa ubora na kujitolea jambo lililosababisha wakapoteza mchezo huo.

Alisema Yanga ina kikosi kizuri na inachotakiwa kufanya ni kujua kuwa michuano ya kimataifa ni tofauti na ligi ya ndani.

“Inatakiwa wachezaji wasiishi kwa historia au mazoea kwani mpira unabadilika na wachezaji wanabadilika pia.

“Inatakiwa wachezaji wabadilike na wajue mashindano ya kimataifa ni tofauti na ligi, wakishatofautisha hilo basi wana nafasi ya kutoboa katika mashindano hayo.

“Niliangalia ile mechi yao lakini wachache waliocheza kwenye kiwango bora na kuonyesha walichonacho lakini wengi ilikuwa tofauti, walifanya makosa ambayo hapa ndani unaweza usiadhibiwe lakini mechi kama hizi za kimataifa watakuadhibu

“Muhimu watambue mechi za kimataifa zinahitajika nguvu za ziada za kupambana uwanjani tofauti na ligi ya ndani,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti