Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele Afungukia Ishu Yake na Hennock Inonga

Mayele Inonga Mayele Afungukia Ishu Yake na Hennock Inonga

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SHAMBULIAJI Mpya wa Yanga Mkongomani Fistoni Mayele, amesema kuwa yeye na Beki Mkongomani wa Simba Hennock Inonga ni washkaji wakubwa sana.

Wawili hawa wameiteka mitandao ya kijamii kwenye Dabi ya Kariakoo kutokana na jinsi ambavyo walipambana kwenye mchezo huo.

Inonga alionekana kumpania zaidi Mayele asiifunge timu yake, huku akisindikiza nje wakati anatoka uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Makambo.

Mayele amesema kuwa Inonga ni mshikaji wake mkubwa wana wanajuana muda mrefu “Inonga ni rafiki yangu sana na hatujawahi kucheza timu moja ila huwa tunakutana kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

“Mimi na yeye tunajuana sana na ni mshikaji wangu, hii ilikuwa kazi na ni lazima kila mmoja aonyeshe kiwango chake,” alisema mshambuliaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live