Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxime matumaini kibao Ihefu

IMG 5260 Mecky Maxime.png Maxime matumaini kibao Ihefu

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Ihefu, Mecky Maxime amesema kwa sasa timu hiyo ipo tayari kwa kuendelea na mapambano ya Ligi Kuu Bara huku akiweka wazi lengo lao msimu huu kama benchi la ufundi ni kufanya vizuri kutokana na ubora wa kikosi kizuri ilichonacho.

Kikosi hicho kilichoweka kambi jijini Arusha kinajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar huku kocha huyo akieleza kinachompa nguvu zaidi ni utimamu wa wachezaji kwani kila mmoja wao anaonyesha kwa vitendo uwanjani.

“Wachezaji wanaonyesha utayari na wote wamefiti kwenye mfumo, tusubiriane uwanjani kuona matunda ya kambi yetu ya Arusha kwa sababu ndio mtaamini kama safari hii tumejiandaa vizuri kukabiliana na kila mpinzani aliyekuwa mbele,” alisema.

Kocha huyo wa zamani wa Kagera Sugar aliongeza, wanafahamu kurejea kwa ligi ushindani utakuwa ni mkali kutokana na timu zote kupata muda mwingi wa maandalizi, huku akieleza suala la wao kushuka daraja halipo na halitatokea.

Katika michezo 14 ambayo timu hiyo imecheza imeshinda mitatu, sare minne na kupoteza saba ikiwa nafasi ya 14 na pointi 13 huku ikikabiliwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Februari 12 kwenye Uwanja wa Manungu Complex.

Chanzo: Mwanaspoti