Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxime kurejea kivingine Mtibwa

Mecky Mexime Maxime kurejea kivingine Mtibwa

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kagera Sugar imeianza Ligi Kuu Bara kwa kusuasua ikishinda mchezo mmoja tu na kutoka sare mbili, huku ikipoteza mechi mbili, lakini hilo halijamshtua sana kocha mkuu wa timu hiyo, Mecky Maxime kwani amesema kutokana na ushindani mkubwa uliopo ameamua kukomaa na wachezaji kuweka sawa kabla ya kurejea tena kivingine.

Kagera kwa sasa inashika nafasi ya 11 na pointi tano kama ilizonazo Singida Big Stars na Dodoma Jiji, lakini zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa na Maxime amesema anarekebisha dosari zilizojitokeza awali.

Maxime aliiambia Mwanaspoti, kutokana na kuwa na muda mrefu wa kusubiri kurejea kwa ligi baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa kwa timu za taifa kulingana na kalenda ya Fifa, ameamua kuongeza dozi ili mambo yaweze kwenda sawa.

“Ni muda mwingi kwa mchezaji wa kibongo kukaa tu, lakini mimi nimetumia nafasi hiyo kurekebisha panapovuja,” alisema Maxime.

Maxime alisema mchezo ujao utakaopigwa Alhamisi ya Oktoba 19 dhidi ya wenzao Mtibwa Sugar ‘Tamtam Derby’ kwenye Uwanja wa Manungu watapambana kupata matokeo ili kujiongezea pointi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live