Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxime awapongeza wachezaji kwa kuzifunga Simba, Azam

Mecky Maxime Press Kocha wa Kagera Sugar, Meck Maxime

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Kagera Sugar, Meck Maxime ametabiri mchezo dhidi ya Dodoma Jiji utakuwa mgumu huku akiwapongeza wachezaji wake kwa kufunga magoli matano dhidi ya Azam, Simba na Geita ambazo zimewakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuchezwa saa 2:15 usiku katika uwanja wa Jamhuri jijini hapa.

Kagera imetoka sare dhidi Simba 1-1 Azam 2-2 na Geita 2-2 michezo yote ikifanyika katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Kagera Sugar ina pointi 24 inashika nafasi ya sita kwenye msimamo, imeshinda michezo sita,imepoteza sita,sare sita,ina magoli ya kufungwa 20 na kufunga 20 imecheza michezo 18.

Akizungumzia na Waandishi wa Habari leo Desemba 29, 2022, Maxime amewashukuru wachezaji wake kwa kuweza kufunga magoli matano dhidi ya timu zilizoshiriki mashindano ya kimataifa.

“Tumetoka kucheza mechi za aina gani tumetoka kucheza mechi na timu ambazo zimetoka kuwakilisha nchi, kwahiyo lazima niwapongeze kuweza kufunga goli tano, nawapongeza sana hayo mengine yanakuja tu na yanarekebishika mazoezini

“Kikubwa kwanza unasifia kizuri ambacho wachezaji wangu wemekionesha halafu hayo mengine yanakuja," amesema kocha huyo.

Akiuzungumzia mchezo dhidi ya Dodoma Jiji amesema anatabiri utakuwa mgumu lakini timu itakatumia nafasi ndiyo itakayoibuka na ushindi.

“Kikubwa tunajua tunakuja kukutana na mchezo wa aina gani Dodoma Jiji wameimarika mchezo utakuwa mgumu kikubwa mwenye kutumia nafasi nafikiri ndio ataibuka na ushindi,” amesema

Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo, Hamis Kiiza amesema; “Tunajua mechi haitakuwa rahisi kwa ajili ukiangalia mechi iliyopita walipoteza na wapo nyumbani, tunajua wajibu wetu tunahitaji kukaa kwenye nafasi gani tupo tayari kupambana ili tupate matokeo mazuri”

Chanzo: Mwanaspoti