Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxime atahadharisha Ligi Kuu

Mecky Mexime Ihefu Kocha Mecky Maxime

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ihefu FC tayari ipo jijini Arusha ilikohamishia makazi yake kutoka Mbarali Mbeya huku Kocha wa kikosi hicho, Mecky Maxime, akisema watarudi na moto Ligi Kuu Bara ikirejea kwa kuwa wanataka kumaliza nafasi za juu.

Inadaiwa Ihefu imenunuliwa na kigogo mmoja wa serikali na maskani yake kwa asa yatakuwa jijini Arusha.

Katika dirisha dogo ambalo rasmi lilifungwa usiku wa kuamikia leo Jumanne (Januari 16), tayari Ihefu ilishakamisha usajili wa Manu Labota kutoka FC Lupopo ya Congo, Joash Onyango, Bruno Gomes, Elvis Rupia, Marouf Tchakei, Kevin Nashon na Aboubakary Khomein wote kutoka Singida Fountain Gate.

Pia inaelezwa wakati wowote timu hiyo itamstambulisha kocha wa zamani wa Mbeya City na Singida United, Mathias Lule, ili kusaidana na Kocha Mkuu, Maxime.

Maxime amesema tayari wameshaanza mazoezi kwenye makao yao mapya jijini Arusha na wachezaji wote wana ari kubwa.

“Tunashukuru tumefika salama Arusha na kupokelewa vizuri na wakazi wa hapa na naamini watatupa ushirikiano ligi ikirejea na tunawaahidi hatutawaangusha.

“Asilimia kubwa wachezaji wapo hapa na baadhi tu bado hawajawasili kutokana na dharura, lakini naamini hadi mwisho wa wiki kikosi kitakuwa kimekamilika,” amesema Maxime.

Alisema anamini wachezaji walioongezwa kikosini wataongeza chachu ya kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo.

“Hatuko katika nafasi nzuri, lakini naamini ligi ikirejea tutakuja kivingine na tutahakikisha tunapambana kadri ya uwezo wetu ili kuleta ushindani na ili kusogea nafasi za juu.

“Uwezo tunao na tuna wachezaji wazuri ambao kama wakijitoa na kuipambania timu, tunaweza kutoka nafasi tuliyopo na kupanda juu na ikiwezekana hata kupata nafasi ya kucheza kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live