Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxime apangua wawili akiivaa Yanga

Kagera 2.jpeg Maxime apangua wawili akiivaa Yanga

Sun, 13 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amefanya mabadiliko ya kikosi chake kitakachoivaa Yanga leo muda mfupi ujao katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kagera Sugar inaikaribisha Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa kuanzia saa 10 jioni huku akifumua kikosi kilichocheza mchezo wa mwisho dhidi ya KMC na kushinda bao 1-0.

Katika kikosi hicho kilichocheza na KMC Novemba 1, Maxime amewapumzisha Yusuph Mhilu na Apollinaire Ngueko raia wa Cameroon ambao wataanzia benchi.

Nafasi zao leo zimechukuliwa na kiungo Ally Nassoro Iddy 'Ufudu' na mshambuliaji, Anuary Jabir aliyeingia kipindi cha pili na kuifungia bao pekee la ushindi dhidi ya KMC.

Maxime leo ameanza na kipa Said Kipao, mabeki wa pembeni Datius Peter na David Luhende (C), mabeki wa kati Laurent Alfred na Abdallah Mfuko, viungo ni Abdallah Seseme, Nassoro Iddy 'Ufudu' na Ally Ramadhan 'Kagawa' huku mawinga ni Meshack Mwamita na Mbaraka Yusuph na Anuary Jabir akisimama mshambuliaji wa kati.

Wachezaji wa akiba ni Ramadhan Chalamanda, Dickson Mhilu, Deus Bukenya, Yusuph Dunia, Appolinaire Ngueko, Erick Mwijage, Hamis Kiiza, Yusuph Mhilu na William Edgar.

Chanzo: Mwanaspoti