Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxime ajipa muda Dodoma Jiji

Mexime Dodoma Jiji Maxime ajipa muda Dodoma Jiji

Mon, 26 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuambulia pointi moja katika mechi mbili za Ligi Kuu, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Mecky Maxime amesema anaamini kikosi hicho kina mwelekeo mzuri na baada ya mechi chache kitaanza kupata matokeo ya kuridhisha na kuwatoa presha mashabiki wake.

Dodoma ilifungua msimu wa 2024/2025 ugenini dhidi ya Mashujaa na kulala 1-0 mjini Kigoma kabla ya juzi usiku kutoka suluhu na Pamba Jiji jijini hapa na sasa itarudi nyumbani jijini Dodoma Septemba 12 dhidi ya Namungo.

Akizungumza na Mwanaspoti, mara baada ya mechi hiyo na Pamba, Maxime alisema katika michezo yote iliyopita walitengeneza nafasi za mabao lakini walikosa umakini kumaliziaji huku akikiri kuwakosa baadhi ya wachezaji ambao bado hawajapata vibali.

Alisema licha ya kucheza ugenini, wachezaji wameonyesha kiwango ambacho kimemridhisha na kumpa matumaini kwamba mechi zinazofuata ikiwemo dhidi ya Namungo wataanza kuvuna ushindi.

“Tulianza mchezo wa kwanza tukiwa chini, lakini tunakwenda tunaimarika na labda nizungumzie kuhusu hizi tuzo za mchezaji bora hebu ziwe na usawa kuna wachezaji wamecheza vizuri lakini tuzo zinaonekana zipo kwamba lazima mchezaji wa nyumbani apate,” alisema Maxime, huku Kocha wa Pamba Jiji, Goran Kopunovic akisema; “Najivunia wachezaji wangu kwa namna wallivyocheza leo kulingana na mpango tuliokuja nao hasa kipindi cha pili tumecheza kwa kasi na haraka, naamini mechi ijayo tukicheza hivi tutakuwa na matokeo mazuri.”

Pamba iliyopanda daraja msimu huu sambamba na KenGold ya Mbeya, hiyo ilikuwa ni suluhu ya pili mfululizo ikiwa nyumbani baada ya awali kufungua msimu na Tanzania Prisons wiki iliyopita.

Chanzo: Mwanaspoti