Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxime aibeza tena kasi ya Yanga Dar

Mexime Picha Data Maxime aibeza tena kasi ya Yanga Dar

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Clezencia TryphoneMore by this Author LICHA ya kikosi cha Yanga kusheheni mastaa kibao wa Kimataifa, sio sababu itakayoifanya Kagera Sugar kushindwa kujinyakulia pointi tatu katika mchezo ujao Jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe timu hizo mbili kwenye mechi zao zilizopita walipata sare ya bao 1-1. Yanga wakicheza na Mbeya City huku Kagera wakiwavaa Gwambina.

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime  alisema; “Majina ya mastaa sio yanayocheza mpira, mpira unachezwa na mguu, mimi hao sijui Fiston sijui nani siwahofii chochote kwanza mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa wote tumetoka kwenye maumivu ya pointi moja.”

Maxime ambaye ni staa wa zamani wa Mtibwa na Taifa Stars, alisema, katika mchezo huo atacheza kwa tahadhari kubwa kwa kutambua mpinzani wake ni kinara katika Ligi na hajakuwepo kwa kubahatisha.

“Kikosi changu mimi nimetoka kudroo, hivyo nimeyaona mapungufu na kuyafanyia kazi, naimani tutafanya vizuri katika mchezo huo, cha msingi wachezaji wangu wanatakiwa kucheza kwa tahadhari na kuwaheshimu Yanga mbali ya kuwa timu kubwa ndio wanaoongoza Ligi,”alisema

Chanzo: mwanaspoti.co.tz