Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxime aanza kujigamba Ligi Kuu

Mecky Maxime Best Coach Maxime aanza kujigamba Ligi Kuu

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 ilioupata Kagera Sugar dhidi ya Mtibwa Sugar, kocha mkuu wa kikosi hicho, Mecky Maxime amesema amefurahishwa na uchezaji wa nyota wa timu hiyo kwani waliyafuata maelekezo yake vizuri kama alivyowaagiza.

Akizungumza nasi, Maxime alisema moja ya tatizo kubwa alilokuwa anakabiliana nalo ni kitendo cha kuruhusu mabao jambo ambalo lilikuwa linamkera hivyo kuweka mkakati mzuri wa kuliondoa na kwa kiasi kikubwa matunda yake yameonekana.

“Sio kwa kiwango kikubwa kwa sababu tangu tumeanza huo mchakato mechi yetu ya kwanza ndio hiyo na Mtibwa tumefanikiwa. Tunahitaji mwendelezo wa hilo kwani itatusaidia hata pale tutakapokutana na mchezo mgumu na tukapata bao moja,” alisema.

Maxime ambaye huo ni ushindi wake wa pili katika Ligi Kuu Bara msimu huu katika michezo sita aliyocheza, alieleza lengo kubwa la timu hiyo ni kushika nafasi tano za juu na hilo litawezekana endapo tu watakuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo.

“Kila mmoja wetu ana malengo yake aliyojiwekea na hivyo pia kwetu. Msimu huu umeanza na ushindani kwa sababu timu zote zimejipanga vizuri. kadri ambavyo ligi inazidi kusonga ndivyo ugumu nao unaongezeka hivyo ni muhimu kujiandaa mapema.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live