Kiungo wa Yanga Maxi Nzengeli amesema hali ambayo inamshangaza kwenye timu yao ni kwamba kila mchezaji ananitaka nafasi ya kucheza mechi ya Leo dhidi ya Simba.
Akizungumza na Mwanaspoti Nzengeli alisema katika mazoezi yao yamekuwa na morali kubwa kwa kila mchezaji akionyesha uwezo mkubwa wa kutaka kucheza mechi ya Leo dhidi ya Simba.
Nzengeli alisema kwenye mazoezi yao kumekuwa na mzuka mkubwa kwenye mazoezi yao ambao umemshtua kwa kila mchezaji kuwa tayari kwa mechi hiyo.
Yanga itakuwa mgeni wa Simba Leo kwenye mechi ya kwanza ya msimu baina ya timu hizo kwenye ligi timu zote zikiwa zinawania pointi tatu kuendelea kujikita juu ya msimamo wa Ligi
"Hii ni mechi kubwa na hali niliyoiona hii wiki mazoezini imenipa uhakika wa hilo kutokana na maandalizi yetu,"alisema Nzengeli mwenye mabao matano katika ligi.
"Kumekuwa na hamasa kubwa baina yetu wachezaji kila mtu unamuona anapambana akiitaka hii mechi kwasisi ambao ni wageni imetupa hamasa kubwa ya kutaka ushindi.
Nzengeli aliongeza kuwa anaamini mbinu za makocha wao na ubora wa wachezaji wenzake utawafanya mashabiki wao kutoka na furaha kwenye mechi hiyo.
Alisema mchezo huo ambao kwake utakuwa wa kwanza kukutana na Simba pale Benjamin Mkapa mashabiki wao wa takuja kwa wingi.