Kiungo wa Yanga, Maxi Mpia Nzengeli amewashukuru viongozi wa Klabu ya Yanga kwa kuifanya siku ya leo kuwa siku yake maalum ikiwa ni mchezo wa kimataifa wa hatua ya awali ya Klabu Bingwa Afrika.
Mchezo huo wa Yanga Sc dhidi ya ASAS Fc umepigwa katika Dimba la Azam Complex, Chamazi na Yanga kufanikiwa kutinga hatua inayofuata kwa kuitungua Asas bao 5-1 huku Nzengeli akitupia bao 2 peke yake na kutoa assist moja ya bao.
Akizungumza kuhusu mchezo huo kupewa jina lake, Max Day, Nzengeli amesema; Ninaawashukuru sana viongozi na mashabiki wa Yanga kwa kuifanya siku ya leo kuwa siku yangu.
"Ni heshima kubwa kwangu sana kwangu na sitaisahau katika maisha yangu. Ninaomba isiishie kwangu tu, ifanyike hata na kwa wachezaji wengine ili kuwapa thamani, kuwapa hamasa na ari zaidi kuipambania timu yao, asanteni Wananchi," amesema Maxi.
Yanga sasa itakutana na Al-Merreikh ya Sudan katika hatua ya pili ya mtoano ambapo mechi ya kwanza itapigwa Rwanda kisha Tanzania.