Wakati wa Dirisha dogo msimu uliopita 2022/23 Simba walifanya usajili wa wachezaji kadhaa katika maboresho ya kikosi chao.
Miongozi mwao ulikuwa ni ujio wa Straika Jean Baleke na kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza.
Wawili hao walifanya vyema ndani ya kikosi cha simba kiasi kwamba mpaka msimu unakamilika kila mtu alikubali kuwa ulikuwa ni usajili Bora kabisa wa Dirisha Dogo.
Drisha hili kubwa la usajili zimefanyika sajili kubwa sana lakini pale Yanga kuna mtu anaitwa Maxi Mpia Nzengeli.
Huyu amegeuka kuwa kivutio kwa uwezo mkubwa anaoonesha na hilo limemuibua Mwandishi wa Michezo kutoka TVE Mbwana Mshindo ambae anasema;
"Kama tulivyokubaliana wakati ule kwamba Baleke na Saido ndio ulikuwa usajili bora wa dirisha dogo, Kwa sasa pia tukubaliane kwamba Max Nzengeli ndio usajili bora wa dirisha hili kubwa. Achana na kina Onana,Tchakei wala Kramo ni Max tu.