Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxi Nzengeli karejea bwana!

Maxi Mpia Nzengeli Ii Maxi Mpia Nzengeli.

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Yanga, Maxi Nzengeli amemaliza ukame wa kucheza zaidi ya dakika 760 bila ya kufunga bao katika mashindano yote kufuatia kuitungua Mashujaa FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, juzi.

Ilikuwa ni raha iliyoje kwa Wananchi wakifurahia chama lao kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kufuatia mabao ya Nzengeli na Mudathir Yahya ambao walilizamisha jahazi la Mashujaa kwa mabao 2-1.

Mara ya mwisho kwa Nzengeli kufunga katika mchezo wa ushindani kabla ya kumaliza ukame huo ilikuwa Novemba 5, 2023 kwenye mechi ya watani wa jadi 'Kariakoo Dabi, ambapo aliweka kambani mara mbili wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 5-1.

Tangu hapo pacha huyo wa Pacome Zouzoua na Stephane Azizi KI kwenye kikosi cha Yanga amekuwa na wakati mgumu kupachika bao katika michezo 10 iliyofuata kwenye mashindano huku upande wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa tisa ambapo amecheza kwa dakika 760 kati ya hizo kwenye ligi ni 415.

Baada ya Mkongomani huyo kufanya balaa kwenye dabi mwaka jana, alicheza michezo mitano kwenye ligi bila kupachika bao ambayo ni dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwa dakika 90, Mtibwa Sugar (dakika 60), Tabora United (dakika 90), Kagera Sugar (dakika 85) na Dodoma Jiji alicheza kwa dakika 90.

Kwa Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Yanga inacheza hatua ya makundi, nyota huyo wa zamani wa Maniema FC ya nyumbani kwao DR Congo alicheza kwa dakika 90 kwenye kila mchezo dhidi ya CR Belouizdad, Medeama nyumbani na ugenini kasoro mchezo mmoja tu ambao ni dhidi ya Al Ahly ya Misri alicheza kwa dakika 75.

Mwishoni mwa mwaka jana, gazeti hili lilifanya mahojiano na kocha wa zamani wa Yanga, Raoul Shungu aliyemtaka kocha wa Yanga, Miguel Gamondi kumpumzisha Maxi ili kurejeshea nguvu ambazo alianza nazo msimu huu.

Shungu aliyeiongoza Yanga hatua ya makundi mara ya kwanza miaka 25 iliyopita kwa sasa anaiona AS Vita ya DR Congo, aliiambia Mwanaspoti kwa njia ya simu kuwa kiungo huyo amekuwa akicheza michezo mingi bila kupumzika hali inayosababisha umakini wake upungue.

Hata hivyo kama muda wa kupumzika nyota huyo amepata kutokana na ligi na mashindano mengine makubwa katika ngazi ya klabu kusimama kutokana na fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika ambazo zinaendelea huko Ivory Coast. Ligi Kuu imerejea na mashindano mengine ya ndani, na nyota huyo anaonekana kurejea kwenye wimbi la upachikaji mabao.

KAZI INGEKUWEPO

Hicho ndicho kipindi ambacho mara nyingi makocha huwa wanawajibika kuhakikisha mchezaji anakuwa kwenye fomu ya upachikaji mabao pamoja na kwamba pia mchezaji naye anatakiwa kujisukuma kwa kujituma kuanzia kwenye uwanja wa mazoezi.

Hakuna mazingira ambayo humuweka mchezaji katika wakati mgumu kama kushindwa kuendeleza kila ambacho alikuwa akikifanya, anaweza kuwa na mawazo ambayo yanaweza kuathiri utendaji, hivyo Gamondi anawajibika kuhakikisha hapotezi mwelekeo.

Msimu uliopita tuliona namna ambavyo kocha aliyepita Yanga, Nasreddine Nabi akikabiliana na mazingira ya namna hii, alihakikisha anatengeneza uwiano mzuri wa kiwango na ndio maana hata pale ambapo alikuwa akikosekana mchezaji fulani alikuwepo mwingine ambaye alitoa ubora uliokuwa ukihitajika.

HIKI KILIMBEBA

Kitendo cha kuona kuwa anatakiwa kufanya zaidi ni miongoni mwa mambo ambayo yalimbeba winga huyo wa kimataifa wa DR Congo na hata alipofanyiwa mahojiano na gazeti hili aliweka wazi.

“Tulitoka kufanya mazoezi makali sana lakini kama mmeona kila mchezo tunabadilika. Tunazidi kuwa wepesi na kila kitu kitarejea kama ambavyo mashabiki wetu wanatamani kutuona tukicheza kama ilivyokuwa nyuma,” anasema.

“Tuko imara sana na ndio maana tumerudi kwenye nafasi ya juu tukiongoza ligi. Hesabu zetu ni kwamba sasa tuendelee kushinda na kukaa pale mpaka tutakapokabidhiwa ubingwa."

HAWA HAPA WADAU

Akimzungumzia mchezaji huyo, Kocha wa timu ya vijana ya Azam , Mohamed Badru anasema: "Maxi ni mchezaji mkomavu. Nilijua tu kwamba anaweza kuondokana na shinikizo la kwamba amepoteza kasi yake ya kufunga mabao, ila mchezaji yeyote anaweza kupitia mazingira ya namna hiyo."

Kwa upande wake, supastaa wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua anasema: "Muda mwingine mchezaji anaweza asifunge, lakini akatoa mchango au msaada kwa mchezaji mwingine. Kiubora nadhani aliendelea kuwa msaada kwa Yanga kwenye safu ya ushambuliaji. Nadhani ambacho kilikosena ni yeye tu kufunga."

NAMBA ZAKE

Kabla ya ukame kumkumba, Nzengeli alikuwa na wastani wa kufunga bao kwenye kila mchezo, kwa maana nyingine unaweza kusema amepachika bao kila baada ya dakika 77 kati ya 541 ambazo alizocheza kwenye mechi zake saba za kwanza za msimu huu Ligi Kuu Bara.

MECHI 3 ZIJAZO

Februari 11. Saa 10:00 jioni

Tanzania Prisons v Yanga

Februari 17. Saa 10:00 jioni

KMC v Yanga

Februari 24. Saa 1:00 usiku

Yanga v CR Belouizdad

Chanzo: www.tanzaniaweb.live