Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxi Nzengeli hakustahili tuzo ya mchezaji bora wa mwezi - Mchambuzi

Fd Nzengeli Gamondi Maxi Nzengeli hakustahili tuzo ya mchezaji bora wa mwezi - Mchambuzi

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini kupitia Kituo cha Televisheni cha TV3, Alex Ngereza amesema kuwa kiungo wa Klabu ya Yanga, Maxi Mpia Nzengeli hakustahili kupewa tuzo ya mchezaji Bora wa mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Ngereza amesema hayo mara baada ya jana Bodi ya Ligi kumtangaza mchezaji huyo raia wa Congo DR kuwa mchezaji Bora wa mwezi huku kocha wa Yanga, Miguel Angel Gamondi akishinda tuzo ya kocha bora wa mwezi.

Nzengeli amecheza mechi mbili za Ligi mwezi Agosti na kufanikiwa kufunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao wakati klabu yake ikishinda mabao 10 katika mechi hizo mbili na kukaa kileleni mwa ligi ikiwa na alama 6.

"Maxi Nzegeli hakustahili kupata tuzo ya mchezaji bora wa mwenzi kwa sababu amefunga magoli mawili na wakati huo Feisal Salum (Fei Toto wa Azam) amefunga magoli matatu kwa maana hiyo tuzo alipaswa kupewa Feisal na sio Maxi Nzegeli," amesema Ngereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: