Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxi Nzengeli afichua siri ya mafanikio

Maxi Mpiah Nzengeli Ms Maxi Nzengeli afichua siri ya mafanikio

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo Maxi Nzengeli amesema kuwa, sababu kubwa ya kufunga akiwa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans ni kuwapa furaha wananchi akiwa ndani ya uwanja.

Kiungo huyo hadi sasa ameshatupia mabao saba, huku akitengeneza pasi mbili za mabao hivyo kahusika kwenye mabao 9 kati ya 25 yaliyofungwa na timu hiyo inayonolewa na Kocha kutoka nchini Argentina Miguel Angel Gamondi.

Katika mabao hayo saba, mawili aliwatungua watani zao wa jadi Simba SC kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi uliochezwa Jumapili (Novemba 05) Uwanja wa Mkapa.

Young Africans leo Jumatano inatarajiwa kushuka uwanjani kusaka alama tatu dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Maxi amesema: “Kikubwa ambacho tunakifanya ni kuwa na mwendo mzuri kwenye mechi ambazo tunacheza.

“Ninapenda kufanya yote kwa vitendo kuliko kuongea sana na hii inanifanya nikipata nafasi ya kufunga nifunge na wakati mwingine kutoa pasi.

“Haya yote ni kwa ajili ya kuwapa furaha wananchi ambao wanajitokeza kwa wingi kwenye mechi zetu ambazo tunacheza waendelee kuwa pamoja nasi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: