Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxi Nzengeli: Sitaisahau 'Maxi Day'

Yangasc Maxi Mzize Aziz Ki Maxi Nzengeli: Sitaisahau 'Maxi Day'

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga wa Yanga, Maxi Nzengeli, ameonyesha furaha yake ndani ya Young Africans baada ya msimu wake wa kwanza kufanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, huku akibainisha kwamba hawezi kuisahau Maxi Day.

Nzengeli aliyejiunga na Young Africans msimu huu akitokea Maniema ya DR Congo, amesema ubingwa uliopatikana kwanza anamshukuru Mungu kwani kulikuwa kuna kupanda na kushuka, bila ya kuwasahau Wananchi kwa sapoti yao.

“Cha kwanza tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwani msimu ulikuwa mrefu sana kupanda na kushuka, tumefurahi kuchukua ubingwa. Matokeo ya ubingwa sio rahisi lakini kitu kikubwa tumeupata ubingwa ni muhimu sana.

“Mimi kitu muhimu kwangu ni kazi, inapotokea sijacheza mechi vizuri nikirudi nyumbani nafanya mazoezi nikiamini kesho nitaenda tena kufanya vizuri kwani Mwenyezi Mungu.

“Nilichojifunza katika mmoja ndani ya Yanga ni kufanya kazi halafu kukaa kimya, lakini pia ushindi huu napenda kumshukuru Mungu kwanza halafu familia na Wananchi.

“Siwezi kuisahau Maxi Day kwa sababu nilikuwa mchezaji wa kwanza kuwa na siku ndani ya Yanga mwisho wa siku leo hii tunafurahi wote tumeupata ubingwa,” alisema Nzengeli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live