Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxi Nzengeli: Mimi sio mfungaji

Maxi Mpia Nzengeli Ii Maxi Nzengeli: Mimi sio mfungaji

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Maxi Nzengeli ameonesha furaha yake baada ya kufunga bao lake la tisa kwenye Ligi Kuu ya NBC ikiwa ni msimu wake wa kwanza ndani ya timu ya Wananchi.

Maxi amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo kati yao yao na Ihefu FC ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 5-0 huku Maxi akifunga bao la tano ambalo hata hivyo limezua mjadala mtandaoni huku baadhi ya mashabiki na wadau wa michezo wakidai kuwa halikuwa bao halali kwani mpira uligonga nguzo ya juu na kurudi ndani lakini refa ataamua ni bao halali.

“Kipindi cha nyumba ni kama nilisimama kufunga kwa sababu ni maisha ya soka, huwezi kufunga kila siku, kuna wakati kama mchezaji unapitia wakati mgumu.

“Mimi sio mfungaji sana. Ni jambo zuri kwa mchezaji wa kati kiungo mshambuliaji kufunga goli sasa nimefikisha magoli tisa nimefurahi kama sifungi kama nafunga bado mimi ni normal na nina furahi.

“Kesho tutajua ni nani tunapangiwa nae wote kwa pamoja tunusubiri tutajua nani tunapangwa nae ila kwa upande wa wachezaji tupo tayari kwa ajili ya robo fainali. Asanteni wanachi kwa kuendelea kutuunga mkono katika michezo yetu yote," amesema Maxi Nzengeli.

Vinara wa magoli LigiKuu Tanzania Bara;

Feisal Salum - 12

Aziz KI - 12

Wazir Jr - 11

Maxi Nzengeli - 9

Mudathir Yahya - 8

Pacome Zouzoua - 8

Marouf Tchakei - 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: