Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxi Nzengeli; Mashine inayorahisisha kazi ya Gamondi pale Yanga

Maxi Nzengeli Msz Maxi Nzengeli

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usajili wa CHAMA pale Yanga kwakuwa ametoka kwa watani zao mitaa ya Msimbazi bado ataimbwa sana PRINCE DUBE kwa kuwa Azam walimchukua Feisal nao Wananchi wameruka na Mwana wa Mfamle kisasi ni haki Wananchi wamelipa.

Atasifiwa STEPHANE AZIZ KI kwa kuongeza miaka mingine ya kusalia Jangwani na Twiga kwa kuwa alimaliza msimu uliopita akiwa kwenye kiwango bora kabisa basi matarajio ni makubwa kuekekea msimu ujao, PACOME ZOUZOUA haachwi kuimbwa kwakuwa Wananchi ndio timu pekee iliyoifunga Al ahly kwenye kampeni za Caf champion league na mfungaji ni Professor kutoka Ivory coast.

Mtamsifia sana JEAN OTHOS BALEKE kwa kuwa hata kabla hajapandishwa kwenye page rasmi za Yanga kama usajili mpya basi wamempandisha kama mfungaji wa goli dhidi ya Augsburg kwa kuwa alitoka pale Kariakoo mitaa ya Msimbazi basi atatrend ila yupo Mwanajeshi mmoja kutoka DR Congo mitaa ya Kindu.

MAXI NZENGELI MPIA hawezi kuwekwa kwenye debate nyingi za wapenda soka ila naamini kwenye kikosi cha Miguel Gamondi ambacho kimesajiliwa kwa gharama kubwa chini ya Muwekezaji Ghalibu Said Mohamed(GSM) Ila anaivaa kofia yenye kengele pale mitaa ya Jangwani na Twiga alipo yeye ndio Yanga ipo ukibisha karudie mechi ya Yanga dhidi ya Augsburg.

Kiwango bora kabisa kwenye mechi kubwa wakati Miguel Gamondi anamuita Chama nje bila kumsahau Aziz ki watu walijiuliza kocha anatoaje wachezaji wakubwa kwenye mchezo mkubwa lakini shughuli nzima alikabidhiwa MAXI NZENGELI na akakiongoza kikosi chake vilivyo.

Max Nzengeli ni moia kati ya wachezaji wanaoipa faida yanga kutokana na energy yake kubwa akiwa uwanjani Max anarahisisha kazi kwenye eneo analocheza hasa uwezo wake wa kuzuia na nakushambulia ndiomaana unaweza usimuone kwenye magoli au assist lakini kazi anayofanya Max Nzengeli pale Jangwani imetukuka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live