Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxi, Aziz Ki tayari kuwavaa Al Ahly

Gamondi Yanga Yake Kazi imeanza ASFC, Yanga, Simba zapewa vibonde

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Yanga ikiwa ni pamoja na Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoah, Zawadi Mauya, Kibwana Shomari wapo kamili kuwavaa Waarabu wa Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na kete ya kwanza wakiwa ugenini walipoteza dhidi ya Waarabu wa Algeria.

Kwa sasa wachezaji wao wapo kwenye maandalizi kuelekea kwenye mchezo wmingine dhidi ya Waarabu wa Misir ambao ni Al Ahly unatarajiwa kuchezwa Desemba 2 Uwanja wa Mkapa.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.

“Wachezaji wanatambua umuhimu wa mechi za Ligi ya Mabingwa na kile ambacho kinatakiwa ni pointi tatu hivyo watapambana kufanya vizuri na kuwapa burudani mashabiki.

“Kukosa matokeo kwenye mchezo wa mwanzo haina maana kazi imekwisha hapana ni muda wa kujipanga upya na kufanyia kazi makosa ambayo tulifanya kwenye mechi zilizopita,”.

Mchezo uliopita wakiwa ugenini walishuhudia ubao ukisoma CR Belouizdad 3-0 Yanga wakapoteza pointi tatu mazima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live