Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxi + Aziz Ki + Pacome = Simba Sc na chenji inabaki

Tano Ta Yanga Maxi + Aziz Ki + Pacome = Simba Sc na chenji inabaki

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota watatu pekee ndani ya kikosi cha Yanga, Maxi Nzengeli, Aziz KI na Pacome Zouzoua, wameonekana kuwa tishio zaidi katika kufunga magoli na kuzifunika timu 14 katika Ligi Kuu ya NBC msimu huu ikiwemo Simba.

Mastaa hao watatu peke yao, jumla wamefunga magoli 18 kati ya 25 yaliyofungwa na timu yetu baada ya kucheza mechi 8 ambazo ni sawa na dakika 720 ndani ya Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2023-2024.

Mpaka sasa, rekodi zinaonesha kwamba, Maxi amefunga magoli (7), Aziz Ki (7) na Pacome (4). Idadi hiyo ya magoli, inafanya kuifunika Simba jumlajumla ambao wenyewe timu nzima wana magoli 17.

Wachezaji wetu wengine waliofunga magoli katika Ligi Kuu ya NBC msimu huu ni Mudathir Yahya (2), Kennedy Musonda (2), Dickson Job (1), Yao Attohoula (1) na Hafiz Konkoni (1).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live