Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxi, Aziz Ki, Job wawania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Yanga

Aziz Maxi Job WA0019 Maxi, Aziz Ki, Job wawania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Yanga

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viungo washambuliaji wa Yanga, Maxi Nzengeli, Aziz Ki na beki wa timu hiyo, Dickson Job wametangazwa kuwa ndiyo wachezaji watatu wa kikosi hicho wanaowania tuzo ya mchezaji Bora wa Timu wa mwezi Oktoba.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi, Oktoba 28, 2023 na Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar.

Wachezaji wote watatu wamekuwa nguzo kubwa ya ushindi ndani ya Yanga wakiaminiwa na kocha wao, Miguel Gamondi kuanza katika kikosi chake.

“Baada ya kuingia mkataba na NIC, uongozi wa Yanga uliunda kamati maalum ya kufanya Tathmini ya mechi zote za mwezi husika na kutupatia majina matatu ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora kisha sisi tutayaanika kwa wananchi kwaajili ya kuwapigia kura.

“Yafuatayo ni majina matatu ambayo kamati imeyaleta kwa uongozi wa Yanga Kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Mwezi, nayo ni Stephane Aziz Ki, Dickson Job pamoja na Max nzengeli, majina haya yatapigiwa kura kupitia Application yetu ya YANGA APP," amesema Kamwe.

Maxi mpaka sasa amefunga mabao matano ya Ligi na assist 2, wakati kinara akiwa Aziz Ki mwenye mabao 6 na assist 1 katika michezo 7 waliocheza sambamba na hatrick aliyowafunga Azam FC.

Job amefunga bao moja lakini amekuwa akisaidia kwa kiasi kikubwa ulinzi wa timu yake ambayo mpaka sasa imefunga mabao 20 na kuruhusu mabao 4 pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live