Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Max Nzengeli azua hofu Yanga

Maxi Nzengeli Mpia Chamazi.jpeg Max Nzengeli azua hofu Yanga

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya imeanza msimu kwa kishindo ikitoa vipigo vizito vya 5G katika mechi tatu mfululizo, jambo linalozua presha kwa wapinzani, lakini habari nyingine ya kuogopesha ni kwamba licha ya kuwa ndio kwanza imecheza mechi sita za michuano tayari nyota tisa wametupia mabao 19.

Balaa ni kwamba kati ya wafungaji kuna mastraika, viungo hadi mabeki jambo linalomaanisha pale Yanga yeyote anakufunga na hiyo sio habari njema kwa wapinzani.

Nyota wapya tangu wametua wameimbwa sana kutokana na vitu wanavyofanya uwanjani kuanzia beki wa kulia, Yao Kouassi aliyefunga bao moja na kutoa asisti moja, kiungo Pacome Zouzoua ‘Profesa’ aliyetupia mabao mawili na winga Maxi Nzengeli ambaye ndiye kinara akiwa na mabao manne katika michezo yote aliyocheza.

Achana na beki mwenye mapafu ya mbwa, Yao. Achana na ufundi wa kuuchezea mpira wa Pacome, yupo mtu mbadi sana, Maxi ambaye mabao yake ni balaa zito.

Kiungo huyo mshambuliaji kutoka DR Congo amefunga mabao manne yakiwa ni kwenye Ligi Kuu Bara na mengine kama hayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika sawa na Stephanie Aziz KI aliyetupia manne akianzia mechi za Ngao ya Jamii, lakini ya Maxi yameshtua zaidi.

Kwenye mabao matatu kati ya manne Maxi ameanza kuyatengeneza mwenyewe kisha kwenda kumalizia kwa kufunga akitangulia kuwachezesha wenzake kuwapoteza umakini wapinzani.

Maxi amefunga bao kwa kichwa dhidi ya Asas ya Djibouti katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya mtoano wa awali wakati Yanga ikishinda mabao 5-1, bao alilolifunga dakika ya saba akipokea krosi ya winga mwenzake Jesus Moloko, huku mengine matatu akiyafunga kwa mguu wa kulia.

Kwenye mchezo huohuo pasi ndefu kutoka kwa kiungo Salum Abubakar katikati ya uwanja ilimkuta beki wa kushoto Nickson Kibabage aliyemwekea pasi safi Maxi akaiweka kwa straika Clement Mzize akipiga pasi ndogo ya nyuma ikamkuta Maxi aliyepiga shuti la chinichini la mguu wa kulia lililojaa wavuni akifunga bao la tano dakika ya pili kati ya tano za majeruhi.

Akili kubwa ya Maxi ni jinsi alivyopiga pasi na kwenda kuichukua mbele, wepesi uliowachanganya Asas wakielekeza akili kwa Mzize huku muuaji akiwa Mkongomani huyo.

Kitu kama hicho akaja kukifanya kwenye mchezo dhidi ya JKT wa Ligi Kuu Bara ambapo katika dakika ya 79 kiungo Khalid Aucho alipokonya mpira katikati ya wachezaji wawili wa wapinzani kisha akampa pasi Nzengeli aliyekimbia na mpira hadi mbele ya eneo la hatari akaachia shuti kali kipa John Mwanda akapangua.

Maxi hakuishia hapo, alikimbia na kuukuta mpira uliotemwa na kipa huyo kisha kufunga kirahisi akiwaacha mabeki watano wa JKT wamesimama kiungo huyo akifunga bao la nne.

Akili hiyo hiyo akaifanya tena dakika ya 88 alipoanzisha shambulizi akiwa nusu ya eneo la Yanga akapiga pasi ndefu kwenda pembeni kulia ilikomkuta Yao naye akakimbia nayo kidogo kisha kugongeana ‘one-two’ na Mzize kisha beki huyo akaingia nao na kumkuta Maxi ndani ya eneo la hatari akiwakimbia mabeki watano wa JKT waliozubaa wakikaba kwa macho, kisha kuwafunga kiulaini katika lango tupu huku kipa ameshapotea marikiti.

Kama hujui muda aliotumia kuupiga mpita kutoka nusu ya eneo la Yanga ikiwa ni kama mita 70 na kitu hadi kufika langoni mwa JKT na kufunga ni sekunde 10 tu, kwani aliupiga dakika 87 na nukta 16 kisha akafika lango mwa Maafande hao dakika ya 87.26 na kufunga nukta moja iliyofuata.

Kasi hiyo ya Maxi kufuata mipira na kushambulia lango la wapinzani, imeelezwa na baadhi ya wachezaji aliokutana nao akiwamo Hassan Nassor Maulid ‘Machezo’ wa JKT kuwa jamaa hakabiki, Awesu Awesu wa KMC alikaririwa kwamba Maxi ni balaa unapokabiliana naye.

Hata beki wa Asas, Gilbert Kaze aliyewahi kuichezea Simba alikiri Maxi anasumbua mabeki na makipa kwa vile mpira ulio nao yupo na pia ni mwepesi kumtoroka adui kabla hajajua cha kufanya, huku Machezo akisema ni ngumu kumnyang’anya.

MSIKIE SHUNGU Kocha wa AS Vita ya DR Congo, Raoul Shungu ameyaona mabao yaliyofungwa na Maxi na kusema wala hashangazwi, kwani ni aina ya mabao aliyokuwa akifunga hata alipokuwa kwao na huo ndio ubora ambao ulimpa heshima Ligi Kuu ya DRC.

Ukiacha yale mabao manane yaliyofungwa na Maxi na Aziz Ki, kiungo Pacome Zouzoua, washambuliaji Clement Mzize, Hafiz Konkoni, Kennedy Musonda kila mmoja amefunga mawili, wakati Mudathir Yahya, Yao na Dickson Job wametupioa moja moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live