Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawakili wa Eto'o wamtetea kesi dhidi yake

Mawakili Wa Eto'o Wamtetea Kesi Dhidi Yake Mawakili wa Eto'o wamtetea kesi dhidi yake

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Mawakili wanaomwakilisha Samuel Eto'o, rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot), wamekanusha kuwa mshambuliaji huyo wa zamani amearifiwa kuhusu kesi za kisheria dhidi yake.

Katika taarifa, kampuni ya mawakili ya Ufaransa ya Vey & Associes ilitupilia mbali madai yaliyotolewa dhidi ya mchezaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 42 kama "uvumi mbaya", na kuongeza kuwa Eto'o hajafahamishwa kuhusu hatua zozote za mahakama au kupewa aina yoyote ya wito.

Wakati ripoti za vyombo vya habari zilidai Ijumaa kuwa Mchezaji huyo Bora wa Afrika mara nne anakabiliwa na hatua inayohusishwa na tuhuma za kupanga matokeo, waraka wa polisi wa Cameroon ulizungumzia madai ya "matumizi mabaya ya mamlaka, rushwa" na madai mengine ambayo hayakutajwa.

Ripoti hizi za polisi zinaonekana kutegemea taswira iliyorekebishwa ya hati inayoonekana rasmi.

Ingawa BBC imeona picha hiyo, bado haijaweza kupata uthibitisho wa uhalisi wake kutoka kwa mamlaka nchini Cameroon.

Hali ya Eto'o hali ' ni mbaya zaidi' kuliko Rubiales

Hii si mara ya kwanza kwa rais wa Fecafoot Eto'o kutiliwa shaka hivi majuzi.

Wiki iliyopita, kundi la maofisa wa kandanda nchini Cameroon walituma barua ya wazi kwa Fifa wakidai kwamba shirikisho hilo "lilikaa kimya" kuhusu tuhuma zilizotolewa dhidi ya Eto'o licha ya "malalamiko na vikumbusho vingi kutoka kwa washikadau wa soka wa Cameroon".

Waliotia saini barua hiyo ni pamoja na mjumbe wa kamati kuu ya Fecafoot Guibai Gatama pamoja na rais na makamu wa rais wa Ligi ya Soka ya Kitaalamu ya Cameroon, shirika linaloendesha mashindano ya ligi nchini humo.

Ikidai kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona, ​​Inter Milan na Chelsea "anaendelea kujitwika kiti cha urais kinyume cha sheria cha Fecafoot", barua hiyo ilisema hali hiyo "pengine ni mbaya zaidi" kuliko kesi inayomhusisha rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Uhispania Luis Rubiales na mshindi wa Kombe la Dunia na Jenni Hermoso, ambayo ilisababisha Fifa kumsimamisha Rubiales kwa siku 90 na kuanzisha kesi za kinidhamu dhidi yake.

Chanzo: Bbc