Sat, 12 Aug 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mbunge wa Dodoma Mjini (CCM), Anthony Mavunde ameahidi kununua kila bao la ushindi la Timu ya Dodoma Jiji kwa Sh300,000.
Lengo la kufanya hivyo ni kuipa hamasa timu hiyo ili ifanye vizuri kwenye mashindano ya msimu wa 2023/24.
Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo ametoa ahadi hiyo usiku wa leo Jumamosi, Agosti 12, 2023 wakati wa hafla ya uzinduzi wa jezi mpya za msimu wa 2023/24 za Dodoma Jiji.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live