Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde: Tulikesha na Eng. hersi kumsubiri Aucho

Aucho Mavunde Aucho na Mavunde.

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanachama wa Klabu ya Yanga, Anthony Mavunde amesema kuwa wakati wa usajili wa kiungo mkabaji, Khalid Aucho, yeye pamoja na Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said walikesha kumsubiri Mganda huyo.

Mavunde amesema kuwa, hayo yalitokana na ugumu wa namna ya kumpata mchezaji huyo akitokea Masr El Makasa ya nchini Misri.

"Hii ni siku ya mwezi Agosti 2021, ambayo Khalid Aucho alisaini kuichezea Yanga. Ni siku ambayo mimi na Eng. Hersi Said tulikuwa macho mpaka alfajiri kuhakikisha kama kweli Aucho anakuja Tanzania kuichezea Yanga.

"Wakati akiwa katika hatua za mwisho za maandalizi ya siku ya safari yake kuja Tanzania. Aucho alipokea ofa kubwa kuliko ile ya Yanga ambayo kibinadamu angeamua kukubali na kubaki Misri, hakuna ambaye angelaumu.

"Mimi nilikata tamaa ya kumpata huyu mchezaji, Eng. Hersi Said alinirudishia matumaini baada ya kufanya mawasiliano na mchezaji kwa simu kwa muda mrefu na kumjenga mchezaji na kumuaminisha timu anayokuja ni timu kubwa na itampa mafanikio.. Naiheshimu sana karama ya mawasiliano ambayo mwenyezi Mungu amemjalia Eng. Hersi Said, alilifanya jambo gumu kuwa rahisi.

"Nilimuheshimu sana pia Aucho kwa uungwana na ustaarabu wake wa kuheshimu makubaliano ya awali na Yanga na aliahidi kwamba atakuja Tanzania.

"Mpaka muda wa ndege unakaribia tulipoteza mawasiliano, hivyo hatukuwa tunajua kwamba amefanikiwa kusafiri au laa. Alivyotua Tanzania alfajiri ndio mimi na Eng. Hersi tukarejea kupumzika.

"Aucho akasaini Yanga na akawa mchezaji wa Yanga na amekuwa mtu muhimu sana katika timu. Leo (Wiki iliyopita) niko hapa kukutakia heri ya kumbukumbu ya kuzaliwa rafiki yangu Dr. Khalid Aucho, mwenyezi Mungu akujalie kheri na baraka tele," amesema Anthony Mavunde.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: