Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavitu yote Yanga fundi ni huyu

Taibi Lagrouni. Kocha Taibi Lagrouni.

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa Yanga mpaka sasa hawamdai kitu kocha wao Miguel Gamondi, akifanikiwa kuibadilisha timu hiyo ikicheza kwa ubora mkubwa. Lakini Gamondi kwenye mdomo wake amempa sifa Kocha wa viungo, Taibi Lagrouni.

Yanga inacheza soka gumu ambalo limewapa shida timu zote zilizokutana nazo msimu huu kukiwa hakuna timu iliyofanikiwa kuinyanyasa kwa umiliki wa mpira kwenye michezo yao 9 waliyocheza kwenye mashindano yote.

Yanga ya Gamondi licha ya kutumia mfumo uleule wa aliyemtangulia Nasreddine Nabi wa 4-2-3-1 lakini Muargentina huyo ameifanya Yanga kucheza soka la moja kwa moja kuelekea mbele zaidi kwa pasi za haraka.

Achana na pasi za haraka Yanga imekuwa haitaki mpinzani amiliki mpira kwa muda mrefu na hakuna aliyefanikiwa kwenye hilo nidhamu ambayo imetokana na kuiva kwa mazoezi ambayo kocha wao wa viungo Taibi Lagrouni.

Lagrouni ameifanya Yanga kuwa timu ngumu kuchoka uwanjani wakiwa na pumzi ya kukaba kwa nguvu wakianzia mbele lakini pia kucheza kwa umiliki mkubwa wa mchezo kwa pasi nyingi ambazo zinatokana na falsafa ya bosi wake Gamondi.

Yanga ikiwa mazoezini imekuwa ikipokea mazoezi makali kutoka kwa Lagrouni ambaye ni kocha wa zamani wa RS Berkane ilipochukua ubingwa wa Shirikisho Afrika ambapo tayari kazi yake imeifanya timu hiyo kuwa tayari.

Gamondi amesema ni mmoja ya wasaidizi wake anayeendelea kuthibitisha ubora wake ndani ya kikosi hicho ambapo kazi yake imewasaidia wachezaji wa timu hiyo kuimarika kutokana na mifumo yao.

“Namjua kwa muda mrefu ni kocha mzuri mwenye uzoefu mkubwa wa kuwandaa wachezaji, kwangu mimi ni mmoja kati ya msaidizi wangu ambaye amesaidia kuwaimarisha wachezaji wetu hapa,”alisema Gamondi.

Vifaa vyashushwa

Katika kuimarisha kazi ya Lagrouni mabosi wa Yanga nao wameshusha vifaa kibao vya mazoezi kambini Jijini Dar es Salaam ambavyo ni mahitaji ya kocha huyo raia wa Morocco.

Vifaa hivyo vya kumpimia kasi ya mchezaji jinsi gani amekimbia ndani ya uwanja lakini pia vifaa vya kufanyia mazoezi tofauti vimeshushwa kambi ya Yanga ambavyo vilihitajika na makocha hao.

Kocha na winga wa zamani wa Yanga Said Maulid ‘SMG’ mbali na kusifia mabadiliko makubwa ya Yanga iliyochini ya Gamondi lakini alipongeza kazi bora ya Lagrouni akisema kocha huyo amewaimarisha wachezaji wa timu hiyo wakionekana kuwa fiti kwenye mechi zao.

“Tunaweza kumsifia Gamondi anastahili hilo kwa kuwa timu ina ubora mkubwa na falsafa yake imekubalika kwa wachezaji akizisdha timu nyingi alizokutana nazo lakini hapohapo lazima tumpongeze kocha wao wa mazoezi ambaye mpaka sasa huwezi kuona watu wanalalamika kwamba timu haipo fiti,” alisema Maulid.

“Yanga inakaba kwa haraka wanakulazimisha upoteze mpira ili waumiliki wao lakini pia wanashambulia na kucheza pasi nyingi huwezi kuyafanya haya kama wachezaji wako hawako fiti.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: