Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauya ana balaa lake huyo!

Gamondi Mauya7 WA0001 Ndani ya dakika chache Mauya anafanya makubwa

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ingawaje kiungo mkabaji wa Yanga, Zawadi Mauya anapewa dakika chache za kucheza, lakini amefanya kazi nzito kwenye mechi ngumu ambazo Yanga inakuwa inahitaji ulinzi zaidi.

Katika mechi sita iliyocheza Yanga, Mauya amecheza nne na jumla ya dakika 99, lakini mechi hizo hazikuwa rahisi kwa timu yake na alisaidia kuwatibulia wapinzani wasisogelee lango la timu yake.

Japokuwa Yanga ilishinda mabao 5-0 dhidi ya KMC, ndani ya dakika 17 alizocheza Mauya alifanya kazi kubwa ya kuzuia mashambulizi ya hatari kutoka kwa wapinzani wao na kusaidia kipa Metacha Mnata kupata ‘Cleen Sheet’ katika mchezo huo.

Yanga ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC mechi ambayo ilikuwa ngumu na ushindani mkali, Mauya alicheza dakika moja, dhidi ya Ihefu dakika 74 na timu yake ilipoteza kwa bao 2-1 na Azam FC amecheza dakika saba, Wanajangwani wakishinda 3-2, mchezo ambao ulikuwa mgumu na ushindani mkali.

Kwa msimu huu hadi sasa mechi ambayo Mauya alicheza dakika nyingi (74) ni dhidi ya Ihefu, ambapo jicho la kiufundi la wadau limeona kitu kwake.

Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kila mchezaji anayekuwepo kwenye timu anakuwa na umuhimu wake kwenye na matumizi yake.

“Kwenye soka hakuna dakika chache, kwani kupitia dakika chache lolote linaweza likatokea iwe ushindi ama kushindwa, mchezaji ndani ya dakika chache anapimwa alichokifanya, ndio maana Mauya ndani ya muda anaopewa anafanya vitu vikubwa,”alisema.

Hoja yake iliungwa mkono na mchezaji wa zamani wa Yanga, Fredy Mbuna aliyesema kila dakika kwa mchezaji ina maana kubwa ni namna ya kuzitumia ili kulinda heshima ya kiwango chake.

“Kinachoangaliwa ni kile alichokifanya uwanjani, mchezaji anaweza akacheza dakika tano lakini zikawa na faida kubwa kwa timu yake,”alisisitiza Mbuna.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: