Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauricio Pochettino: Bado nipo sana

Mauricio Pochettino 4842395 Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino

Fri, 1 Mar 2024 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Chelsea, Mauricio Pochettino Carabao amesema kuwa wamiliki wa klabu hiyo wamekuwa wakimpa ushirikiano tangu timu hiyo ilipofungwa na Liverpool katika Fainali ya Kombe la Ligi ‘CARABAO CUP’.

Pochettino alikosolewa baada ya Chelsea kupokea kichapo cha bao 1-0 baada ya muda wa nyongeza dhidi ya Liverpool dhaifu katika mchezo uliofanyika Jumapili (Februari 25).

Amesema alikuwa na mazungumzo chanya na wamiliki wenza, Todd Boehly na Behdad Eghbali.

“Wameonesha ushirikiano na baada ya mchezo ule, baada ya Todd kunitumia ujumbe mzuri,” amesema Pochettino.

“Niliwasalimia wamiliki nilipowaona nikiwa uwanjani na baadae nilikutana na Behdad na tulikuwa na mazungumzo mazuri.

“Tulibadilishana mawazo kuhusu mchezo na nafasi tulizoshindwa kufunga mabao na kushindwa kutwaa taji kwa sababu nafikiri tulicheza vizuri sana wakati wa dakika 90.”

Mchambuzi wa Sky Sports na beki wa zamani wa England, Gary Neville alielezea Chelsea kama timu isiyo na uwezo.

Akijibu kuhusu maoni ya Neville, Pochetino amesema: “Katika miaka mitatu au minne pamoja na Jurgen Klopp, Liverpool haijawahi kushinda taji. Sasa wamepata kile walichokistahili.”

Pochettino amesema mshambuliaji Christopher Nkunku, amecheza mechi mbili tu za Ligi Kuu msimu huu, alitoka majeruhi.

Chelsea, ambayo iko katika nafasi ya 11 katika msimamo wa Ligi Kuu, inakaribia zaidi katika upande wa kushuka daraja kuliko nne bora.

Chanzo: Dar24