Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maulid Kitenge: Simba wasitishike na "Atmosphere" ya Uwanjani

Maulid Kitenge Atoa Rai Maulid Kitenge

Wed, 26 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba wakikutana na kila aina ya vitisho kuelekea mchezo wao wa marudiano ugenini dhidi ya Wydad Casablanca.

Mwandishi wa Michezo Mkongwe, Maulid Kitenge nae ametoa rai yake kwa Simba SC kuelekea mchezo huo.

Akizubgumza Maulid anasema;

“Casablanca ni mji wa wapenda mpira na wanazipenda timu zao, kwa hiyo moja Ya vitu ambayo Simba watakutana navyo ni ile Atmosphere ya uwanjani kwanza inakuchanganya.

“Taifa hapa walikuwa wachache wakawasha kama ‘kimoto’ hivi sasa ile ndo inakuwa uwanja mzima unalipuka.

“Mimi niwaambie Simba, wasitishike na hali ambayo watakutana nayo, vitimbi vitakuwa vingi lakini focus yao ibaki katika dakika 90.

“Wana mtaji wa bao 1 wanahitaji sare, wapambane wasifunguke sana, wacheze kwa kuheshimu wapinzani na wajue wako ugenini, wasiruhusu goli la mapema,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live