Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matusi yamponza Aussems, FKF yamchunguza

Aussems+pic Kocha wa AFC Leopards, Patrick Aussems

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Kandanda nchini Kenya FKF limeanzisha uchunguzi dhidi ya kocha mkuu wa AFC Leopards Patrick Aussems kufuatia lugha ya matusi kwa mwandishi wa habari pamoja na kuwaita maofisa KPL kuwa vichekesho.

Aussems ambaye ni kocha wa zamani wa Simba ya Tanzania alisema maneno hayo baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya KPL dhidi ya Nzoia Sugar uliomalizika kwa sare tasa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari alimuita mwandishi mmoja aliyemuuliza swali kuwa ni ‘mpuuzi’ na kuwaita maofisa wa mchezo huo kwamba wamechezesha kama vituko “wanachekesha”.

Afisa habari na masoko Pharis Kimaru alisema shitaka hilo limefika kwenye kamati ya nidhamu ya FKF.

“Tunakuja na maamuzi sawa na kitendo chake, uchunguzi ukikamilika ndani ya siku chache zijazo”, alisema Mtendaji Mkuu wa shirikisho la soka nchini humo Barry Otieno.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live