Nyota wa Barcelona Miralem Pjanic anaripotiwa kuwa kwa sasa ana matumaini ya mwanzo mpya baada ya kuwasili kwa Xavi kama meneja mpya Barcelona.
Pjanic alijikuta analazimika kuondoka kwa mkopo kwenda Besiktas, ambako yupo sasa akianza msimu wake vyema baada ya changamoto za majeraha siku za hivi karibuni.
Nyota huyu mwenye miaka 31 aliwasili Barcelona mwaka 2020, ikiwa ni sehemu ya dili la kubadilishana wachezaji lililomuhusisha Arthur Melo pia.
Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, Pjanic sasa ana matumaini mapya juu ya hatma yake na klabu ya Barcelona.
Pjanic ni mmoja ya watu wanaomkubali zaidi Xavi, na anaamini atapata nafasu ya kumshawishi meneja huyu baada ya kumalizana na dili lake la mkopo huko Besiktas.
Xavi kwa upande wake ameshawaahidi wachezaji kuwa yey vigezo vyake vitakuwa ni ubora pekee, na hakuna jambo jingine. Ikiwa staa huyu atapata nafasi ya kumshawishi basi huenda akapewa nafasi ya kuthaminiwa zaidi Barca.