Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matumaini kibao kwa Rasmus Hojlund

Rasmus Hojlund Rasmus Hojlund

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag ana matumaini kwamba Mshambuliaji wake Rasmus Hojlund atafunga tu mabao, hivyo mashabiki wanatakiwa kuwa na subra.

Hojlund alishindwa kucheka na nyavu dhidi ya Sheffield United katika ushindi wa mabao 2-1 mwishoni mwa juma lililopita iliyopita huku akiendelea na ukame wa mabao Ligi Kuu England.

Aidha Mshambuliaji huyo bado anasubiri kufunga bao lake la kwanza kwenye ligi tangu alipojiunga akitokea Atalanta dirisha la usajili la kiangazi kwa Pauni 72 milioni.

Licha ya kusuasua kwenye ligi Mshambuliaji huyo amefanya vizuri katika mechi zake mbili za kwanza za Ligi Mabingwa Ulaya didi ya dhidi ya Bayern Munich na Galatasaray kwani ameweka kambani mabao matatu mpaka sasa kwenye michuano hiyo.

Kocha Ten Hag amesema: “Kwanza kabisa, inabidi tufanye kazi za kawaida, amekosa mechi za kujiandaa na msimu, mechi nne za kwanza, lakini nadhani tangu alipokuja amekuwa na mchango mkubwa.

“Tumejenga utaratibu na hilo litampa muda zaidi na kufanya maamuzi bora kwa malengo zaidi, lakini mabao dhidi ya Galatasaray yalikuwa ya uwezo vilevile hata dhidi ya Bayern Munich.

“Nadhani ni mchezaji ambaye atacheza katika safu ya ushambuliaji yetu kwa muda mrefu. Nina amini atafunga hata kwa upande wa Marcus Rashford.”

Hojlund alikuwa na wakati mgumu wakati anakipiga Copenhagen kwani alifunga mabao matano kabla ya kuuzwa Sturm Graz kutoka Austria.

Chanzo: Dar24