Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matukio yaliyosimamisha Siku ya Mwananchi Yanga

CC2971D3 8B54 41CC 8F05 889B24AEB791.jpeg Matukio yaliyosimamisha Siku ya Mwananchi Yanga

Sun, 7 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Achana na matokeo ya Yanga kufungwa 0-2 na wageni wao Vipers FC, ukweli ni kwamba, Wananchi jana walifunika katika suala zima la kuhitimisha kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi.

Kabla ya Yanga kupoteza mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Vipers, zilifanyika burudani kadhaa ikiwemo utambulisho wa mastaa wa kikosi hicho.

Miongoni mwa wachezaji walioteka shoo wakati wa utambulisho, ni wachezaji wapya akiwemo Stephane Aziz Ki na Bernard Morrison.

Aziz Ki ambaye amejiunga na Yanga akitokea ASEC Mimosas, alikuwa mtu wa mwisho kutambulishwa na kushangiliwa kwa shangwe kubwa uwanja mzima.

Kabla ya Aziz Ki, alitangulia Morrison ambaye alianza kwa kuwaomba radhi mashabiki wa Yanga akisema: “Nisameheeni, najua niliwaudhi wakati naondoka. “Niliwahi kusema kwamba nimeenda Simba ambapo ni chuo kikuu cha soka Tanzania, sasa niwaambie kwamba nimerudi Yanga kuja kusomea masters, hiki ndiyo chuo kikubwa zaidi.

“Nimefurahi kuona kocha mkubwa Afrika, Pitso Mosimane yupo hapa, nimwambie tu, amekutana na Kocha Bora wa Tanzania, Nasreddine Nabi.” Baada ya kuzungumza hayo, Morrison aliibua shangwe uwanja mzima ambapo mashabiki walimshangilia na kuonesha kwamba wamemsamehe.

Wengine walioibua shangwe wakati wa kutambulishwa ni Yannick Bangala, Feisal Salum, Fiston Mayele na Gael Bigirimana.

SAPRAIZI YA MANARA

Wakati wengi wakifahamu kwamba Haji Manara ambaye amefungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na kukutwa na hatia juu ya masuala ya kinidhamu, jana alifanya sapraizi ya kutosha.

Wakati Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikitoa adhabu kwa Manara Julai 21, mwaka huu, ilisema hatakiwi kujihusisha na masuala ya soka, hivyo hatakuwepo katika Tamasha la Mwananchi, lakini jana aliibuka.

Manara aliingia uwanjani akisindikizwa na walinzi, kisha akachukua jukumu la kutambulisha kikosi cha Yanga kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji, kisha akaaga akisema anaondoka kwani alialikwa kuwa mshereheshaji tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live