Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matukio ya Kihistoria Dabi ya Kariakoo; Simba aliwahi kupigwa 9-0 na Yanga

Yanga Yarudi Kileleni Matukio ya Kihistoria Dabi ya Kariakoo; Simba aliwahi kupigwa 9-0 na Yanga

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Haya hapa Matukio na vipigo vikubwa zaidi kuanzia 5+ kwenye derby ya Kariakoo

FT' Yanga Sc 9 - 0 Simba Sc (1938)

FT' Yanga Sc 5 - 0 Simba Sc (1968)

Dilunga ⚽⚽

Zimbwe⚽⚽

Kitwana ⚽

▪️MNYAMA MPIRA KWAPANI: 3 March 1969 :

Simba waligoma kurejea uwanjani kipindi cha pili baada ya kufungwa (3-0). Yanga walipewa pointi (3) na mabao (3) mezani.

▪️FT' Simba Sc 6 - 0 Yanga Sc (1977)

Sanga ⚽ OG

Kibadeni⚽⚽⚽

Masimenti ⚽ ⚽

▪️MKUBWA ASAIDIWA: 1988 Yanga Sc waliwasaidia watani zao Simba SC wasishuke daraja, Mchezo wa mwisho wa ligi kuu', Yanga wakishinda wanatwaa Ubingwa, Simba wakisare au kupoteza wanashuka daraja.

Yanga Sc hawakumkaba kwa makusudi, Hamisi Shikamkono ili afunge goli Simba wasalie ligi kuu.

Shikamkono akafunga goli, Simba Sc wakasalia ligi kuu na Yanga wakaukosa Ubingwa. Msimu huo Simba SC walikuwa na mgogoro mkubwa baina ya katibu mkuu, Jimmy David Ngonya na wazee wa klabu hiyo.

Mpaka sasa Simba na Yanga zinaendekea kuwa Miongoni mwa timu ambazo hazijawahi kushuka daraja ligi kuu Tanzania tangu ianzishwe.

▪️YANGA SC WAAZIMA WACHEZAJI SIMBA SC

1998 Yanga SC waliazima wachezaj kutoka Simba SC ili waongeze nguvu kikosini kwao kwenye michuano ya CAF champions league ambapo Yanga ndio walikuwa klabu ya 1 East Africa kuingia group stage.

Wachezaji walioazimwa ni, Zamani hawakuwa maadui

✅Monja Liseki

✅Shabani Ramadhani

✅Alphonce Modest

▪️FT' Simba Sc 5 - 0 Yanga Sc (2012)

OKwi ⚽⚽'

Sunzu ⚽

Kaseja ⚽ (Penati)

Mafisango ⚽ (Penat)

▪️FT' Simba Sc 1 - 5 Yanga Sc 2023

Kibu ⚽️

Musonda ⚽️

Max ⚽⚽️

Aziz Ki⚽️

Pacome ⚽️ (penati)

Yanga inaongoza kwa kumfunga Simba mara nyingi wakati Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa viatu hii ilikuwa1949 ilipocheza na kombaini ya jeshi la majini Navy ya Afrika Kusini.

Yanga ndiyo iliyochukua ubingwa mara nyingi zaidi (29) kuliko timu yoyote wakati Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa jezi hii ilikuwa 1938 ilipocheza na kombaini ya mabaharia wa meli zilizotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam.

Yanga ndiyo timu ya kwanza kutinga robo fainali ya CAF champions league mwaka 1969 (dhidi ya Nkana Red devils) wakati simba ndiyo timu ya kwanza kupanda ndege mwaka 1963 walienda Ethiopia kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo.

Yanga ndiyo inaongoza kwa idadi ya magoli yaliyofungwa kwenye mechi za Simba na Yanga wakati Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa suti hiyo ilikuwa ni mwaka 1974 ilipokwenda Poland

Je, unajua kwanini kipigo cha 2023 kwa Simba Sc kinauma sana ? Yaani wale waliokuwa wadogo enzi za Simba Sc akishinda 5 dhidi ya Yanga mwaka 2012 sasa hivi wamekuwa wakubwa na wamekishuhudia kwa Ukubwa zaidi, hata mimi mwenyewe.

Je, kipigo kikubwa Kinachofuata kitakuwa lini na goli ngapi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live