Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matthijs de Ligt kutimkia Man Utd

Skysport De Matthijs De Ligt 6392783 Matthijs de Ligt kutimkia Man Utd

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: Dar24

Manchester United inataka kumsajili beki wa FC Bayern Munich, Matthijs de Ligt, dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa kile kinachoelezwa staa huyo hana furaha kwenye kikosi cha ‘The Bavarians’.

Beki huyu mwenye umri wa miaka 24 ana uhusiano mzuri na kocha wa Man United, Eric ten Hag kwa sababu ndiye alikuwa kapteni wa timu wakati kocha huyo anaifundisha Ajax.

Inaelezwa De Ligt hana furaha kwa sababu hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Munich, msimu huu akiwa amecheza mechi 16 tu za michuano ambazo nyingi aliingia akitokea benchi.

Man United iliwahi kutaka kumsajili de Ligt dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2019, kabla hajajiunga na Juventus akitokea Ajax.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

Chanzo: Dar24