Kocha msaidizi klabu ya Simba, Selemani Matola, amesema uzembe mdogo wa safu yao ya ulinzi umewagharimu kwenye mchezo wao wa juzi dhidi ya Tanzania Prisons na kujikuta wakipokea kipigo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Matokeo hayo yaimefanya Simba kufikisha pointi 36 baada ya kushuka dimbani mara 16 ikishika nafasi ya tatu mbele ya Azam FC wanaoongoza msimamo na Yanga iliyopo nafasi ya pili.
"Ni matokeo ya mpira, tumecheza vizuri lakini makosa ya mabeki wetu yametugharimu, tunaenda kufanyia kazi makosa yetu na kurejea kwenye ubora wetu, tulitengeneza nafasi nyingi tumeshindwa kuzitumia na wenzetu wamepata nafasi chache wamezitumia, tunawapongeza," amesema Matola.